HATUA NNE MUHIMU ZA KUFUATA ILI UWEZE KUANZA KUINGIZA FAIDA YA SHILINGI LAKI TANO KILA MWEZI KUPITIA BIASHARA YA SABUNI ZA ASILI

 


Kama wewe ni miongoni  wahitimu/ wanafunzi wa elimu ya juu ambaye una ndoto ya kumiliki biashara ambayo itakuwa inakupatia faida ya kuanzia silingi laki tano au zaidi kila mwezi, una karibishwa sana kusoma makala hii hadi mwisho. Kwani kupitia makala hii nitakuonesha HATUA TANO MUHIMU ZA KUFUATA ILI UWEZE KUTENGEZA FAIDA YA TZS 500,00/ KILA MWEZI KUPITIA BIASHARA YA SABUNI ZA ASILI. 

Kabla ya kukuleza hatua hizo muhimu za kufuata naomba nianze kwa ufupi sana nikueleze ninaposema sabuni za asili ninamaanisha kitu gani?

Sabuni za Asili ni Nini? 

Hizi ni sabuni ambazo zina viambato (ingredients) vitokanavyo na mimea ya asili ambyo huzifanya sabuni hizo kuwa na uwezo wa kufanya ngozi iwe na muonekan mzuri bila kuiathri. Najua wengi wenu hasa akina dada (wanawake) mtauwa mmesikia kuhusu sabuni za mchele, manjano ukwaju, kahawa n.k. zote hizi ndio zinajulikana kama sabuni za asili. 

Sabuni hizi hutumiwa na watu kwa sababu mbalimbali kama vile kungarisha mwili (kufanya uwe mweupe), kuondoa madoa usoni, kuondoa harara, kufanya ngozi ionekane nyororo na kadhalika.  Kinachozifanya sabuni hizi ziitwe za asili ni kutokana na ukweli kwamba kwenye sabuni hizi, kinachofanya ngozi iwe na muonekano mzuri ni madini yaliyopo kwenye mimea iliyotumika katika kutengeza sabuni hizo na siyo kemikali kama ilivyo kwenye sabuni za kawaida. 

Baada ya kupata uelewa (japo kwa ufupi) kuhusu maana ya sabuni za asili, sasa naomba turudi kwenye mada yetu ya msingi kuhusu HATUA TANO MUHIMU ZA KUFUATA ILI UWEZE KUTENGEZA FAIDA YA TZS 500,00/ KILA MWEZI KUPITIA BIASHARA YA SABUNI ZA ASILI. 

HATUA YA KWANZA:  CHAGUA MZALISHAJI AMBAYE ATAKUWA TAYARI KUKUUZIA SABUNI ZA ASILI KWA MFUMO UJUliKANAO KAMA "CONTRACT MANUFACTURING"

Njau utakuwa unajiuliza nini maana ya uzalishaji wa biadhaa kwa mkataba. Huu ni mfumo wa uzalishaji wa bidhaa ambao unatumiwa na wafanyabiashara makini ulimwenguni ambapo mfanyabiasra anakuwa anazalisha bidhaa na kuizua sokoni kwa lebo yake ilihali yeye hana hata kiwanda cha kutengeza bidhaa hiyo. 

Mfumo huu unafanya kazi kama ifuatavyo:-

Nitatoa mfano ufuatao ili kukuonesha jinsi ambavyo mfumo wa uzalishaji wa bidhaa kwa mkataba (contarct manufacturing) unavyofanya kazi. Kwa mfano mfanyabiashara A anataka kuzalisha sabuni za mchele lakini kwa bahati mbaya hana mashine wala muda wa kuzalisha bidhaa hiyo. Anachokifanya anamtafuta mfanya biashara B ambaye yeye yupo tayari kwenye soko la uzalishaji wa sabuni za mchele wnakubaliana jinsi ambavyo mzalishaji B atakuwa anamzalishia bidhaa mfanyabiashara A. Wakikubaliana mwisho wa siku mzalishaji B ataanza kumzalishia bidhaa mfanyabiashara A na kumruhusu mfanya biashara A aweke lebo yake yeye mwenyewe na kuipelekea sokoni bidhaa hiyo iikiwa na lebo yake. 

Faida za kutumia mfumo huu

Kwa ujumla mfumo huu una faida kubwa sana kwa yeyote anayeanza biashara kwa kuwa:-
  1. Hauitaji muda mwingi wa kufanya usimamizi kwa kuwa unachofanya wewe unatoa mahitaji kwa mwenye kiwanda mliyekubaliana tayari na yeye anakuletea bidhaa zako zikiwa tayari;
  2. Hauitaji mtaji mkubwa  kwa kuwa hauitaji kuwa na mashine yeyote zaidi ya pesa kidogo tu za kuweza kutoa oda ya kutengenezewa bidhaa
  3. Unapata fursa ya kujifunza/ kujaribu kuhusu biashara fulani kabla ya kuamua kufanya uwekezaji mkubwa . Maana yake ni kwamba hata kama una pesa za kutosha sio vizuri sana kuwa unakurupuka kufanya uwekezaji mkubwa kwa kununua mashine za uzalishaji wa bidhaa. ikitokea biashara hiyo ambayo umewekeza pesa nyingi ikawa hailipi maana yake unakuwa umekula hasara kubwa. (na hii ndio sababu kubwa wajasiliamli wengi hapa Tanzania huwa hawaendelei ni kwa kuwa kila anayeanza anataka aanze akiwa na mashine yake) 

Mfumo huu ni maarufu sana kwa wafanyabiashara katika nchi kama za chi kama China lakini kwenye nchi zinazoendela kama Tanzania bado mfumo huu haujaenea sana. Hapa kwetu kuna baadhi ya wafanyabiashara makini kama vile Mo ambaye utaona anzo bidhaa mbalimbali kama vile boda boda, TV na fiji zikiwa zinauzwa madukani kwa jina la Mo (mfano Mo electronics) ambazo kimsingi yeye hana kiwanda cha kutengeza bidhaa hizo lakini ametengenezewa na makamuni ya nje kwa utaratibu wa contact manufacturing

Najua ni ngumu sana kwa hapa Tanzania kupata mwenye kiwanda ambaye atakubali kukuzalishia bidhaa kwa utaratibu huu (si unajua wabongo tuna wivu na hatupendi kuona mtu akifanikiwa). Pamoja na kuwa sio rahisi kupata kampuni ambayo inaweza kukushika mkono na kuanza kukuzalishia bidhaa kwa jina lako hpa nchini kwetu, bado kuna makapuni macache sana kama vile Kunyumba Natural Products ambalo hutoa fursa kwa mjasiliamli yeyote yule ndani ya Tanzania anayetaka kuanza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwa utataribu wa "Contarct Manufacturing". Bidhaa ambazo mpaka sasa unaweza kuzalisha kwa utaratibu wa contract manufacturing kupitia Kampuni ya Kunyumba Natural Products ni hizi zifuatazo:-
  1. SABUNI ZA KUOGEA ZA ASILI (MCHELE, MANJANO, UKWAJU, KAHAWA N.K)
  2. SHAMPOO ZA AINA MBALIMBALI
  3. MAFUTA YA NAZI (VIRGING COCONUT OIL)
  4. MAFUTA YA NYWELE
  5. FACIAL SERUM
  6. SABUNI ZA KUNAWIA MIKONO (HAND WASH SOAP)
  7. SABUNI ZA KUDEKIA 
  8. SABUNI ZA CHOONI
  9. LOTION ZA ASILI 
  10. PEANUT BUTTER 
Kama unahitaji kuanza kuzalisha bidhaa yeyote kati ya hizo nilizozitaja hapo juu kwa utaratibu wa contarct manufacturing kupitia Kampuni ya Kunyumba Naural Products tafadhali wasiliana nasi kwa KUTUANDIKIA UJUMBE WA WHATSAPP KWA SIMU NAMBA  0752026763. 

HATUA YA PILI: WEKA DHAMIRA YA KUANZISHA BIASHARA ULIYOAMUA KUANZA KUIFANYA 

Dhamira ya biashara yako ndio kitu ambacho kitakufaya udumu kwenye soko na kuweza kupata mafanikio katika biashara yako. Inashuriwa kwamba dhamira ya kuanzisha biashara iwe ni kutataua tatizo fulani lililoko kwnye jamii yako kwa mfano dhamira ya biashra yako. Kwa mtu mwenye ndoto ya kutengeza faida ya TZS 500,000 kila mwezi dhamira yake inaweza kuwa hii ifuatayo:-

 "KUWASAIDIA WANAWAKE NA VIJANA WASIO NA AJIRA KATIKA ENEO LAKO KUPATA KIPATO CHA KUWAWEZESHA KUMUDU MAHITAJI YAO YA MSINGI KUPITIA UUZAJI WA SABUNI ZA ASILI"  
Hii ni dhamira nzuri kwa mtu mwenye ndoto ya kuwatumia vijana waliopo katika eneo fulani katika kusambaza/kuwafikishia wateja bidhaa yake kwa kuwa inakurahisishia kuwapata watu ambao watakusaidia kufanya bidhaa yako iwafikie wateja kwa urahisi (Ntakounesha jinsi ya kuwatumia hao watu katika hatua ya tano) 

HATUA YA TATU: WEKA MALENGO YA MUDA MFUPI YA BIASHARA YAKO

Malengo ni kitu muhimu sana katika biashara kwani ndicho kitu ambacho kitakusukuma katika kufanya mambo katika biashara yako. kKitu cha kuzingatia katika kuweka malengo ni kuhakikisha kuwa malengo yako yanakuwa halisia na ili kufanya hilo ni vizuri ukaanza na malengo ya muda mfupi. Mfano ufuatao unaonesha jinsi ambavyo malengo yanapaswa kuwa;


LENGO KUU: Kuanzisha biashara ya sabuni ya asili ambayo baada ya miezi mitatu (3) itakuwa inaniingiza faida ya TZS 2,000,000/= kila mwezi ili niweze kukidhi mahitaji yangu ya msingi.

HATUA YA NNE: ANDAA MKAKATI WA KUTEKELEZA MALENGO YAKO


Hii ni hatua muhimu sana katika kuanzisha biashara kwa kuwa bila kuwa na mkakati mzuri wa namna ya kutekeleleza malengo uliyoyaweka inakuwa ni kazi bure. Na wajasiliamali wengi sana wamejikuta wanashindwa kufanikiwa kwa kuwa hawana mkakati madhubuti ya kufikia malengo waliyojipangia.  

kutokana na umuhimu wa mkakati wa utekezaji wa malengo uliyoyojiwekea nimeandaa mwongozo wunaoonesha mfano wa mkakati ambao unapatika kwenye nakala laini (soft copy) BUREE KABISA

BOFYA HAPA SASA KUPATA MWONGOZO WAKO SASA (BUREE)


 

Maoni

  1. Thanks for sharing about four important steps to follow though business of natural soaps. A healthy lifestyle entails taking proper care of the body and skin. You can also check out about cosmetic products manufacturer here.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JINSI YA KUMILIKI BIASHARA YA SABUNI ZA UREMBO ZA ASILI ZENYE BRAND YAKO KWA MTAJI USIOZIDI ELFU 50,000 TU